Waandamanaji hao wamekuwa wakisisitizia ulazima wa kuhitimishwa vita na mauaji ya kimbari ya Israel katika Ukanda wa Gaza ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kupelekwa katika ukanda huo ambapo ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa, hali ya kibinadamu ni mbaya mno.
Maandamano hayo yamekuwa yakifanyika hata ndani ya Marekani kwenyewe ambapo serikali ya Biden imeendelea kutoa na uungaji mkono wa hali na mali kwa utawala ghasibu wa Israel.Mbali na Marekani, nchini Uingereza pia taifa jingine linalouunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel katika mauaji yake huko Gaza, mamia ya watu walaindamana jana na kukusanyika mbele ya ofisi za serikali katika mtaa wa Downing wakati Waziri Mkuu wa nchi hiyo alipokuwa katika mazungumzo na Kamalla Haris, Makamu wa Rais wa Marekani. Maandamano kama hayo yameshuhudiwa nchini Tunisia na Jordan ambapo waandamanaji wamelaani jinai na mauaji ya Israel dhidi ya wananchi wa Gaza huko Palestina na kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kuhitimisha mauaji hayo. Baadhi ya mataifa mengine ambayo yameendelea kushuhudia maandamano ya kulaani jinai za Israel ni Malaysia, Indonesia, Pakistan, India, Afrika Kusini, Nigeria na Ufilipino.
342/